Picha: Baraka Da Prince Amdhalilisha Linah Ukumbini, Anaswa Akishika Kifua cha Linah - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Picha: Baraka Da Prince Amdhalilisha Linah Ukumbini, Anaswa Akishika Kifua cha Linah

Baraka na Linah waliokuwa miongoni mwa mastaa waliokuwa kwenye ratiba ya kuburudisha siku hiyo, walifanya tukio hilo walipokuwa nyuma ya jukwaa (back stage) walipokuwa wakisubiri muda wao wa kutumbuiza ufike.

Paparazi wetu aliyekuwa akifanya ziara ya kushtukiza mara kwa mara back stage, kuna wakati alifanikiwa kumkuta Baraka akiwa ameingiza mkono kwenye kifua cha Linah huku mrembo huyo akionekana kumpa ushirikiano.

“Mh! Huu ni udhalilishaji, hata kama wameamua kuwa na uhusiano, kwa nini haya mambo wasifanyie chumbani? Baraka anamdhalilisha tu Linah. Naye sijui kwa nini anakubali kuingizwa mkono vile,” alisikika shuhuda mmoja.

Alipoulizwa na paparazi wetu kuhusiana na tukio hilo na kama ana uhusiano wa kimapenzi na Baraka, Linah alidai haoni tatizo kwani atakuwa amerejea kwenye himaya yake ya zamani.

“Naona ni bora kumrudia wa zamani ambaye nimemzoea,” alijibu Linah na kuomba aachwe.

Kwa upande wake Baraka ambaye inafahamika ni mpenzi halali wa mtoto mzuri Naj, hakutaka kuzungumzia chochote kuhusiana na tukio hilo zaidi ya kuishia kucheka tu.

Linah na Baraka waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya kila mmoja kuchukua hamsini zake hadi waliponaswa wikiendi iliyopita ufukweni hapo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.