Mose Iyobo: Ninavyoishi na Aunt Ezekiel ni Ndoa Tosha, Ila Tutathibitisha Zaidi. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mose Iyobo: Ninavyoishi na Aunt Ezekiel ni Ndoa Tosha, Ila Tutathibitisha Zaidi.

Dancer maarufu wa Diamond, Mose Iyobo amesema jinsi anavyoishi na Aunt Ezekiel ni ndoa tosha lakini atafunga ndoa ili watu wa verify kama instagram.
Mose Iyobo na Aunt Ezekiel wamefanikiwa kupata mtoto mmoja [Cookie] mwenye umri wa mwaka mmoja.

Akiongea kwenye kipindi cha E News, kinachoruka kupitia EATV, Iyobo alisema, “Lakini ninavyoishinae ni ndoa tosha kwa sababu tunaishi kama baba na mama hivyo nataka kujithibitisha inabidi nifunge ndoa ili watu wani-verify kama instagram.”

Aidha Iyobo ameongeza kuwa hapendi watu wanavyomzungumzia vibaya mzazi mwenzie huyo wakidai kuwa eti ni mzee kwani angelikuwa hivyo yeye asingelisogea kwa kuwa angelikuwa kama anatembea na mama yake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.