Mastaa Waweka Wazi Bei za Malipo yao Mtu Akihitaji Picha Zao Za Utupu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mastaa Waweka Wazi Bei za Malipo yao Mtu Akihitaji Picha Zao Za Utupu.

Dunia imekwisha!  Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mastaa wa kike Bongo ambao wamekuwa vinara wa kuweka picha zao chafu mitandaoni, kuweka wazi viwango vyao vya malipo endapo mtu atahitaji picha zao za utupu (X).
Miongoni mwa wasanii hao ni muuza nyago maarufu Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’,  Asha Salum ‘Kidoa’ na Isabela Mpanda ‘Bella’ ambao kila mmoja amekiri kuwa yupo tayari kupiga dili hilo ili aweze kujiingizia ‘mkwanja’ mnono na kudai kwa sababu wao hawatoshiriki ni picha tu hivyo hakuna ubaya.
GIGY MONEY
“Hee, ninavyoijua pesa jina langu lenyewe linajieleza, sasa nawezaje kukataa dili la hela ikiwa sidhuriki chochote maana kama ni picha zangu kila kukicha natupia mtandaoni, mtu si anaweza kuchukua tu, lakini mpaka kaniomba kaniheshimu itabidi anilipe kama shilingi milioni 50.”
LULU DIVA
LULU DIVA
“Ni kweli napiga picha zisizo na maadili kwa nchi yetu ambazo zinaweza kumshawishi mtu kunipa dili la aina hiyo japo kwa kucheza sipo tayari, ila picha akinipa shilingi milioni 200 nakubali anipige hizo picha.”
kidoaKIDOA

Kwa kuwa hiyo pesa nitakuwa sijaitolea jasho siwezi kuiacha, nikilipwa shilingi milioni 500 napiga hilo dili kwa moyo mkunjufu.”
ISABELA
“Kipindi hiki pesa ilivyokuwa ngumu naanzaje kukataa, kwani ninavyoweka picha zangu huko mtandaoni kuna mtu ananilipa na mbona nasemwa sana, bora nikasemwa nikiwa nimefaidika tena kupitia picha yangu tu tatizo liko wapi, nikipewa shilingi milioni 100 nakubali.”


NENO LA MHARIRI:

Ni vyema wasanii hawa wakazingatia maadili ya Kitanzania kwa kuepuka kupiga picha za utupu kwa namna yoyote. Watafute fedha kwa njia halali kutokana na kazi zao. Waache kuiga mastaa wa nje kama vile Rihanna, Kim Kardashian, Amber Rose na wengineo ambao wamekuwa wakilipwa pesa ndefu kwa kupiga picha hizo ambazo zimekuwa zikitumika kwenye majarida na mitandao mbalimbali.

CHANZO: GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.