Hawa Ndio Washindi Wa Shindano La Mr & Miss Talent University Mkoa Wa Kilimanjaro 2016:Cheki Picha - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hawa Ndio Washindi Wa Shindano La Mr & Miss Talent University Mkoa Wa Kilimanjaro 2016:Cheki Picha

Washindi wa Mr & Miss Talent University mkoa wa Kilimanjaro 2016  wote kutoka chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College
Na Dickson Mulashani
Usiku wa kuamkia Jumapili mkoa wa Kilimajaro ulishuhudia shindano la kumsaka mkaka na mrembo  mwenye kipaji kutoka vyuo vikuu mkoani hapa ambapo chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College kiliweza kung'ara kwa kutoa washindi wote wa kwanza na wakiwa wanafunzi wa shahada ya mawasiliano ya Umma ( Mass Communication).

Katika shindano hilo  jumla ya washiriki 36 ambapo 16 walikuwa ni wasichana na 20 walikuwa wavulana  kutoka vyuo vikuu vya Mwenge Catholic University, MOCU ( Ushirika) , KCMC University, Mweka Wildlife College na  Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCo) walichuana vikali katika kuonesha uhodari wa mavazi na vipaji vyao huku mkali wa muziki Vannessa Mdee akifika kuwapa kampani.

Vannessa Mdee akifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo

Kumi bora kwa upande wa wanaume
Kumi bora kwa upande wa wasichana
Mr & Miss Talent University mkoa wa Kilimanjaro 2016 wakipongezana baada ya kutangazwa washindi


Sehemu ya wadau waliohudhuria katika hafla hiyo

Irene Kijazi mshindi wa Miss Talent University mkoa wa Kilimanjaro 2016 mara baada ya kuvikwa taji hilo


Brian Clement mshindi  wa Mr Talent University mkoa wa Kilimanjaro 2016 mara baada ya kuvikwa taji hilo
Matukio katika picha 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.