Ben Pol Atoa Nafasi Kwa Management Inayotaka Kusimamia Kazi Zake. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ben Pol Atoa Nafasi Kwa Management Inayotaka Kusimamia Kazi Zake.

Mkali wa wimbo ‘Moyo Mashine’ Ben Pol amesema kwa sasa yupo tayari kusaini kwenye label yeyote ambayo itakuwa na nia ya kumpeleka mbali zaidi kimuziki.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Ben Pol amesema label ambayo anahitaji ni ile ambayo itamtoa alipo sasa na kumpeleka katika level nyingine.

“Mimi sasa hivi nakaribisha proposal za management, kama management au label inataka kufanya kazi na Ben Pol iniambie itanifanyia kitu gani, kwa sababu kama kampuni sasa hivi inakuja inaniambia itapeleka nyimbo zangu MTV au wapi sasa hivi mimi nyimbo zangu zinachezwa huko na nilipeleka mwenyewe, hiyo management hainifai kwa sababu hivyo nimeshafanya mwenyewe. Management ikinionyesha kitu ambacho siwezi kufanya kwa sasa tunaweza fanyakazi,”

Bep Pol alisema kwa sasa hana management lakini ana watu ambao anafanya nao kazi kwa ukaribu zaidi ambao pia humshauri mambo mbalimbali kuhusu muziki wake.

-Bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.