Baraka Da Prince Afunguka Kuhusu Yeye na Linah Baada ya Picha Tata Kuzagaa Mtandaoni. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baraka Da Prince Afunguka Kuhusu Yeye na Linah Baada ya Picha Tata Kuzagaa Mtandaoni.

Msanii Baraka da Prince amekanusha vikali kumshika msanii wa kike wa bongo fleva sehemu za kifuani, na kusema aliyepiga picha hiyo aliikuza.

Akiongea kwenye eNews ya East Africa TV, Baraka amesema hajawahi kufanya kitendo kama hicho kwani walikuwa sehemu yenye watu wengi, na pia hajawahi kuwaza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Linah.

“Siwezi kufanya kitu kama hicho kwa sababu pale pana watu wengi, ile picha ilikuwa ya kawaida, yule aliyeipiga na kuipost amekuwa kama kaikuza, sijawahi kufikiria hata kutoka naye”, alisema Baraka.

Pia Baraka amesema siku ya tukio ambayo ilikuwa ni siku ya kuadhimisha miaka 10 ya muziki wa Christian Bella, aliondoka mapema na hakufanya tukio lolote baya.

“Nimetoka kuperfom nikaondoka zangu, sikukaa hata nusu saa, nimemaliza nikaondoka, wasiwe wanaamini mambo ya hivyo”, alisema Baraka.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.