Abdu Kiba: Nipo Tayari Kufanya Kazi na Lebo ya WCB - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Abdu Kiba: Nipo Tayari Kufanya Kazi na Lebo ya WCB

Abdul Kiba amesema yupo tayari kujiunga na lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond kama hela itawekwa mezani.
Bifu la Alikiba na Diamond linaonekana kuathiri mpaka mfumo wa watu wa pembeni wanaowazunguka wasanii hao japo kila mmoja anakubali kuwa hana tatizo na mwenzake huku ukweli wa kila mmoja ukibaki moyoni mwake.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Abdu Kiba alisema kuwa kama watakuwa na pesa za kutosha na makubaliano mazuri anaweza kufanya kazi chini la Label hiyo [WCB].

“Nipo tayari naangalia pesa, kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya kazi na mimi naweza nikafanya kazi chini ya lebo hiyo,” aliongeza.

Siku chache zilizopita Abdu Kiba ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Bayoyo’.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.