Ubora wa Video ya Shetta Kufika Kimataifa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ubora wa Video ya Shetta Kufika Kimataifa

Ubora wa Video ya Shetta Kufika Kimataifa
WADAU mbalimbali wa muziki nchini wamesema ubora wa video ya wimbo wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nurdin Bilali ‘Baba Qayla’ au ‘Shetta’, ‘Namjua’ utafanya vizuri katika soko la kimataifa.

Wadau hao walisema video hiyo imeandaliwa kwa kiwango kikubwa kitakachompa urahisi msanii huyo kujitangaza na kupata shoo za kimataifa tofauti na wasanii wengine ambao hawawekezi katika video za nyimbo zao.

Walisema licha ya kuandaliwa nchini Afrika Kusini katika miji ya Cape town na Johannesburg, lakini namna vitu vya thamani vikiwemo ndege, boti na nyumba za kifahari zilivyotumika vimeongeza ubora wa video hiyo.

Shetta aliwahi kutamba na wimbo wa ‘Shikorobo’ aliomshirikisha msanii wa Nigeria, Kcee.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.