Video: Meneja Wa Trey Songz Na Big Sean, Kevin Liles Afunguka Ukaribu Wake Na Diamond Platnumz - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video: Meneja Wa Trey Songz Na Big Sean, Kevin Liles Afunguka Ukaribu Wake Na Diamond Platnumz

CEO wa kampuni ya KWL Management inayowasimamia wasanii wakubwa wa Marekani wakiwemo Trey Songz na Big Sean, Kevin Liles, amefunguka kwenye Twitter kuhusiana na ukaribu alionao na Diamond.

Kupitia session yake ya #AskKevinLiles, mtanzania aitwaye Sammy Gratian alimuuliza: Is Tanzanian artist, Diamond Platnumz under your management or possibly working with any artist under your management? #AskKevinLiles.”

Kevin alijibu kwa kupost video akielezea kuwa yupo karibu na Diamond kama washkaji.
“Shout outs to my friend Diamond Platnumz and my whole Tanzania crew,” anasema Kevin kwenye video hiyo.
Akaongezea kwakusema anaipenda Tanzania, alishakaa nchini na hata kukutana na Rais mstaafu J Kikwete nakupata chakula cha usiku na Diamond wakiwa NY. “I love the country, I have spent some time there, I met the president, I actually had dinner with Diamond here in New York, I don’t manage him but we always friendly and help each other,” aliongeza.

Alimalizia kwa kusema, “Hey Diamond check out your boy, holla at me right.”
Diamond hakupuuzia ujumbe huo. Alimjibu Kevin kwa kumwandikia: Hey boss, Am Coming to America next Thursday….i will make sure i see you, thanks for your Major Support my boss.”
Hey boss, Am Coming to America next thurday....i will make sure i see you, thanks for your Major Support my boss🙏https://twitter.com/KevinLiles1/status/733737890904199169 
Liles aliwahi kuwa Rais wa Def Jam Recordings na Makamu Mkuu wa rais wa Island Def Jam music group kuanzia mwaka 1999 hadi 2004. Aliwahi pia kuwa Makamu Mkuu wa rais wa Warner Music Group.

-tubongetz

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.