Video: Alikiba aeleza sababu ya M.I kutoonekana kwenye video ya Aje - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video: Alikiba aeleza sababu ya M.I kutoonekana kwenye video ya AjeUnaweza ukajiuliza kwamba kwanini audio ya wimbo mpya wa Alikiba Aje anasikika rapper wa Nigeria M.I Abaga lakini hujamuona kwenye video yake. Alikiba amezungumza na Bongo5 kueleza kwanini imekuwa hivyo.


Amesema audio ambayo ilisambaa wiki hii ikiwa na sauti ya rapper huyo ni demo (ilikuwa haijakamilika). “Tulivyokuwa tumeplan kufanya video na nini ratiba za M.I zilikuwa zipo tight na mimi sikutakiwa kuendelea kuchelewa sababu muda ulikuwa umeenda,” amesema Kiba.
“Kulikuwa na Plan B vilevile ndio nikaweza kufanya nyimbo nyingine, I mean nikaweza kurudia zile verse ambazo M.I alitakiwa afanye ila baada ya mimi kumaliza alituma ile nyimbo na tukaweza kuisikiliza lakini ilikuwa demo, kwahiyo tulikuwa nayo pending mpaka aweze kumaliza shughuli zake ndio tuweze kufanya video,” ameongeza.
“Lakini tukaona tunachelewa na kazi zilipokuwa nyingi, kila mtu ana ratiba zake na nyimbo ilikuwa ya kwangu kwahiyo tukaamua tufanye kitu tofauti, kama ulivyoona nimeimba French katika wimbo ambao nimetoa video yake.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.