Baada ya Kuvunjika Kwa Penzi, Shilole Afunguka "Mpenzi Wangu Ni Hela" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baada ya Kuvunjika Kwa Penzi, Shilole Afunguka "Mpenzi Wangu Ni Hela"

Baada ya kuvunjika kwa mahusiano na Nuh Mziwanda, taarifa za chini zimezidi kuenea kuwa Shilole ana mahusiano ya kimapenzi na msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Nerd aliye chini ya label ya Ommy Dimpoz, PKP.

Akiongea kwenye kipindi cha Busati, kinachoruka kupitia Magic FM, Shilole amesema hana mpenzi kwa sasa.

“Mimi mpenzi wangu ni hela, Nerd ni rafiki yangu. Ukiwa kwenye mapenzi unakuwa kama kipofu unakuwa hauoni. Ukimkabidhi mtu moyo wako anakuwa anaufinyanga, kwa sasa moyo wangu umestawi tofauti na zamani,” aliongeza.

Hata hivyo Shilole amesema hana namba ya Nuh Mziwanda na hajawahi kuwasiliana naye tangu walipoachana. Kwa sasa muimbaji huyo ana wimbo mpya uitwao Say My Name.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.