Richard BBA Afunguka 'Canada Hali Mbaya' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Richard BBA Afunguka 'Canada Hali Mbaya'

Mara nyingi kumekuwa na sintofahamu kwa washindi wa Shindano la Big Brother Africa (BBA) kwa hapa nchini mara tu baada ya kukabidhiwa kitita chao. Wengi wa mashabiki wa shindano hilo wanakuwa na shauku ya kuona maendeleo ya washindi hao kupitia fedha walizopata.

Richard Bezuidenhout ni mshindi wa BBA mwaka 2007, ambaye kwa sasa maisha yake anayafanyia nchini Canada, akiwa na mkewe na watoto wake wawili huku akijiendeleza kimasomo.
Mshindi huyo alifanya mahojiano na gazeti hili moja kwa moja kutoka nchini Canada.

Kwa nini alipotea?
“Sijapotea ila nipo nchini Canada na ndiyo makazi yangu kwa sasa kwa kuwa najaribu kuwapatia vijana wangu maisha bora kama vile elimu na huduma nzuri za afya.”

Nini kilimfanya kuhamia Canada?
“Kikubwa zaidi ilikuwa ni shule kwa kuwa nilikuwa nasoma chuo kimoja kinaitwa NATI (Northern Albert Instute of Technology) na baada ya kumaliza masomo yangu nimeanza kutengeneza filamu kwa ajili ya kuelemisha vijana wenzangu wa Tanzania hali ya maisha huku ughaibuni (Canada) ilivyo mbaya.”

Kuwaelimisha vijana kivipi?
“Vijana wengi wa Kitanzania wanajua huku kuna maisha mazuri na kufikiri mtu akiishi huku ni tajiri lakini kumbe sivyo hata kidogo kwa kuwa huku kuna maskini sana kama huko na kuna wengine wakija huku hawataki kurudi Afrika kwa vile hawana kitu wanaona aibu kabisa.”

Vipi kuhusiana na mkwanja alioshinda BBA aliufanyia nini?
“Wakati nipo Tanzania nilifungua kampuni yangu ya filamu kama nilivyokuwa nimeahidi na nikacheza filamu nyingi tu ikiwepo Fake Smile, Family Tears na nyingine nyingi na matumizi mengine ni ya kwangu binafsi kwa sababu watu wengine hawapendi kuweka mambo yao wazi kwa hiyo mtu unaweza kujiuliza mbona sioni kitu walichofanya washindi wa BBA kumbe mwingine anakuwa hapendi kuweka wazi kila kitu chake.”

Kuna Watanzania huko anashirikiana nao kwenye filamu?
“Ndiyo. Yupo jamaa anaitwa Episcopere Emmanuel ambaye aliandika Kitabu cha Kanumba cha The Great Fallen Tree ambaye anaigiza na kuandika na sasa tunatengeneza Filamu ya Mchumba Siyo ATM Machine.

Vipi kuhusu familia?
“Mimi na familia yangu yaani mke na watoto wangu wawili tupo huku tunaendelea na maisha na ninamshukuru Mungu tunaendelea vizuri.”

Ana mpango gani wa kuwainua waigizaji wa Bongo?
“Tumejipanga vizuri mimi na Epicsropere tutakuja huko Bongo na tutafanya nao kazi pamoja na tukienda vizuri watakuja huku pia.”

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.