Nisher Aingia Kwenye Ugomvi na G Nako baada ya kuipotezea video yake ya ‘Arosto’ na kuirudia na Hanscana, Ishu Nzima Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nisher Aingia Kwenye Ugomvi na G Nako baada ya kuipotezea video yake ya ‘Arosto’ na kuirudia na Hanscana, Ishu Nzima Ipo Hapa

Muongozaji maarufu wa video Tanzania, Nisher ameamua kutoa dukuduku lake baada ya G nako kuipotezea video aliyoitengeneza yeye ya ‘Arosto’ na kwenda kuirudia na director mwingine.

Nisher mfululizo wa video nyingi aliyoweka Instagram Nisher alikuwa analalamika kuwa G nako na Weusi walimwambia video hiyo haiwezi kutoka kwasababu ilikuwa haijafikia viwango walivyokuwa wanataka, lakini cha kushangaza hata alipotaka kuirudia walisema hawana pesa japo yeye aligharamikia video hiyo ya kwanza.

“Huu ni Usaliti! Nataka pesa zangu zirudi Kistaarabu tu. Haya ni maisha na maisha lazima yaendelee” Nisher ameandika kwenye Instagram yake na kuelezea kuwa hawezi umia kwasababu hakuigharamikia video hiyo.

Nisher pia alielezea kuwa mwanzo alimtumia G nako video hiyo private kupitia Youtube ili aione lakini cha kushangaza baada ya muda akakuta tayari imeachiwa mtandaoni na G nako akawa anamshutumu yeye kwa kuivujisha.

Nisher amesema ameshangaa kuona jana G nako anatangaza kuachia video mpya ya wimbo huo huo alishoot yeye mwanzo na director mwingine, Hanscana wakati hajarudishiwa gharama alizotumia kushoot video ya kwanza ambayo waliipotezea, amesema alitumia Million 3 na Laki 9.
Katika Hatua nyingine Nisher Pia ameachia version yake ya video hiyo, Itazame hapa
Na hii ndio version ya video hiyo iliyoongozwa na Hanscana,
Nini Maoni Yako Kuhusu Ishu Hii ?

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.