Lady Jaydee Amtaka Gardner Aombe Radhi Ndani Ya Siku 7 Kwa Kauli Aliyotoa Dhidi Yake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lady Jaydee Amtaka Gardner Aombe Radhi Ndani Ya Siku 7 Kwa Kauli Aliyotoa Dhidi YakeMsanii wa muziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kupitia mwanasheria wake Aman G. Tenga kutoka Law Associates (Advocate) ameandika barua ya kumtaka mtangazaji maarufu wa Clouds Fm, Gardner G. Habash, kuomba msamaha mbele ya umma kutokana na kauli yake ya uzalilishaji aliyoitoa dhidi yake.
Buff Bantam Hen {Gallus gallus domesticus} with nine of her ten chicks, 2-days-old. The tenth chick is under her
Lady Jaydee
Gardner ambaye alikuwa mume wa muimbaji huyo wa Ndindindi, anatuhumiwa kulifanya kosa hilo mnamo tarehe 6 May 2016, akiwa kama mshereheshaji tamasha la Miss TIA 2016 lililofanyika CDS Park (zamani TCC) ambapo alidaiwa kutamka kwa makusudi maneno ya udhalilishaji na kejeli “Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi” mbele ya umma.
Baada ya wiki moja toka tukio hilo litokea, Lady Jaydee kupitia mwanasheria wake ameandika barua hii.
1-6
2-3
3-3-768x677
Licha ya kauli hiyo kupingwa na wadau mbalimbali katika mitandao ya kimajii, pia Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla, alimtaka mtangazaji huyo kumuomba radhi aliyekuwa mke wake, Lady Jaydee kwa ‘kile alichokiita’ kama udhalilishaji kwake na kwa wanawake wote.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.