KAMPUNI YA KIDACHI YA KIBUNIFU IMETENGENZA FRIDGE YA ARIDHINI ISIYOHITAJI UMEME - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

KAMPUNI YA KIDACHI YA KIBUNIFU IMETENGENZA FRIDGE YA ARIDHINI ISIYOHITAJI UMEME


Na John Conor  Bongoswaggz 
Kampuni ya kidachi inayohusika na mambo ya ubunifu, imetengeneza fridge inayochimbiwa chini na isiyohitaji umeme. Fridge hii kubwa yenye umbo kama chombo cha mviringo inaweza kuhifadhi ujazo wa fridge 20 zilizojaa vyakula. Na bado aihitaji umeme. Fridge hii iliyotengenezwa kwa ustadi mkubwa na Floris Schoonderbeek mmiliki na muazishili wa kampuni ya Weltevree inawekwa kwa kuichimbia nchini, nyuma ya nyumba yako.

Fridge hii unayoifukia chini ya udongo kama futi 3 ivi; Inauwezo wa kuhifadhi hali ya ubaridi wa nyuzi joto 10 (10 degrees Celsius) kwa mwaka mzima. Hali hii ya ubaridi inafaa sana kwa mboga, matunda, soda na hata mvinyo ila haifai kuhifadhi nyama au maziwa.Fridge hii imetengenezwa kwa ajili ya wale
watu wenye bustani za mboga, mzizi pika
(root cellar) na matunda; pia wale wanaopenda kunywa mvinyo wenye baridi ya asili. Fridge hii imebuniwa kwa ajili ya watu waliochagua kuishi maisha ya kisasa na yakujitegemea. Watengenezaji wa fridge hii kampuni ya 'Weltevree' inategemewa kuanza kuuza fridge hii ya kipekee kabisa sokoni mwanazoni mwa mwaka 2017.
Fridge hii ya ardhini (groundfridge) inatoa nafasi kwa walimwengu wapya wanaopenda kushughulikia vyakula vyao kwa njia uhuru na kujitegemea wenyewe.

Kwa habari za ubunifu na technologia tafadhali tembelea bongoswaggz.com

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.