Jose Mourinho Atangazwa Rasmi Meneja Mpya wa Manchester United - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jose Mourinho Atangazwa Rasmi Meneja Mpya wa Manchester United

Klabu ya Manchester United leo imemtangaza rasmi Mreno Jose Mourinho kuwa Meneja wao mpya akichukua mikoba ya Mholanzi Louis Van Gaal aliyeo tumuliwa hivi Karibuni.
Mourinho,54, ambaye amewahi kuvifundisha vilabu vya Porto,Chelsea,Inter Milan,Real Madrid, amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwatumikia mashetani hao wekundu.
.
“Kuwa Meneja wa Manchester United ni heshima kubwa . Ni Klabu inayofahamika na kupendwa duniani kote” amesema Jose baada ya kukabidhiwa Mikoba

Mreno huyo ambaye ni mzoefu wa kushinda mataji ataanza rasmi kuitumikia klabu hiyo kuanzia msimu wa 2016/2017.

Jose Mourinho ametangaza rasmi kuwa meneja mpya wa klabu ya Manchester United.

Ametia saini mkataba wa miaka mitatu.

Mreno huyo anachukua nafasi ya Mholanzi Louis van Van Gaal, aliyefutwa kazi Jumatatu siku mbili baada ya kushinda Kombe la Dunia.

“José kusema kweli ndiye meneja bora zaidi wa soka kwa sasa,” naibu mwenyekiti mtendaji wa United Ed Woodward amesema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.