Chadema Kujadili Serikali ya Magufuli - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chadema Kujadili Serikali ya Magufuli

Kamati Kuu ya Chadema itakutana mjini Dodoma katika kikao chake cha kikatiba kuanzia Mei Jumatano na Alhamisi kitakachojadili mwenendo wa Serikali ya CCM chini ya Rais John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene imesema kikao hicho, pamoja na mambo mengine, kitajadili taarifa ya hali ya siasa nchini.

Pia kikao hicho kitajadili na kupitisha mpango kazi wa chama kwa mwaka huu unatokana na Mpango Mkakati wa Chama wa miaka 5 kabla ya Sekretarieti kuanza utekelezaji.

Mpango huo utahusisha shughuli mbalimbali za chama ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa chama nchi nzima na kuendelea kuwatumikia wananchi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.