Alikiba Ala Bonge La Shavu Kutoka Sonny Music South Africa, Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Alikiba Ala Bonge La Shavu Kutoka Sonny Music South Africa, Ipo Hapa

Alikiba baada ya kusaini mkataba huo amewashukuru mashabiki wake kwa support waliompa toka aliporudi na wimbo wake wa 'Mwana' mpaka leo hii na kusema atafanya sherehe na mashabiki zake ili kufurahi nao baada ya kuweza kusaini mkataba na 'Sony Music'

"Nataka kukumbuka nilivyorudi kwenye game 2014 toka nimepumzika, nimepiga hatua kubwa sana na hii ni kutokana na support kutoka kwa mashabiki, mtanisamehe mashabiki pale nilipokosea, ila kwa furaha niliyonayo leo kusaini mkataba huu naomba nikirudi nifanye party ili nifurahi pamoja na mashabiki zangu ambao walikuwa na mimi mwanzo mpaka sasa" alisema Alikiba.

Mbali na hilo Alikiba amewashukuru waandishi wa habari na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vikimpa support kwenye kazi zake za muziki siku zote.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.