Usajili Bado Waendelea Radio EFM Wamnyakuwa Lady Jay Dee, Je Anaenda Kuwa Mtangazaji ? - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Usajili Bado Waendelea Radio EFM Wamnyakuwa Lady Jay Dee, Je Anaenda Kuwa Mtangazaji ?

Wenyewe wanasema ‘Huu Mchezo Hauhitaji Hasira.’

Ni mchezo upi huo? Usemi huu ulianza baada ya EFM kuwapora watangazaji wawili wa Clouds FM, Gerald Hando na Paul James kabla ya wao nao kuporwa mtangazaji wao, Gardiner G Habash.

Na sasa movie linaendelea kunoga. Lady Jaydee anayefahamika kuwa mgogoro mzito na Clouds FM na aliyekuwa mke wa Gardiner, amejiunga na EFM katika mradi ambao ni wao pekee wanaujua kwa sasa.

Sitaki kuamini kama Lady Jaydee anaweza kurejea tena kwenye kazi yake ya utangazaji lakini kwa inavyoonekana, kuna kitu wamepanga kukifanya.

Jaydee alishare picha na video kadhaa zinazomuonesha akitembezwa na kutambulishwa kwenye studio za EFM.

“HuuMchezoHauhitajiHasira #NdiNdiNdi Efm feat Jide,” aliandika Jide kwenye picha moja.

Kila mtu anasubiri kujua nini hasa Lady Jaydee na EFM wamepanga kukifanya.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.