Sina Ndoto Ya Kumuoa Jokate - Alikiba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sina Ndoto Ya Kumuoa Jokate - Alikiba

Bet SasaMwanamuziki nguli wa muziki wa Bongo Fleva anaye tesa na ngoma yake ya Lupela, Ali Kiba, ameshikwa na kigugumizi kuhusiana na mahusiano yake na model maarufu wa hapa nchini, Jokate Mwegelo.


Kigugumizi hicho kimemkuta Alikiba kwenye mahojiano aliyo yafanya na eNewz ya East Africa Television baada ya kusema kuwa yeye na Jokate ni marafiki tu.


Lakini King Kiba alizidi kujibu juu ya ni nani ambaye kwake ni wife material ambapo alifunguka nakusema kuwa "...wazee wetu zamani walikuwa hawakurupuki kutafuta mwanamke wa kuoa, hivyo ili kupata wife material nilazima kuanzia kwenye urafiki kwanza na kisha ndiyo ndoa ifuate".
Maswali yalipo mbananisha kuwa, kama yeye na Jokate ni marafiki hivyo tutarajie siku moja kuja kuona Jokate anakuja kuwa 'Wife materia' wake na hata ndoa....? Ndipo King Kiba aliposhikwa na kigugumizi cha ni nini ajibu nakumalizia kwakusema hana ndoto ya kuja kumuoa Jokate.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.