Sijawahi Kumuona TID Anatumia Madawa ya Kulevya - Billnas - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sijawahi Kumuona TID Anatumia Madawa ya Kulevya - Billnas

Rapa Billnas kutokea Lebo ya Radar Entertainment inayomilikiwa na msanii wa Bongo Flava TID, amesema kuwa hajawahi kumuona TID akitumia Madawa ya Kulevya kama maneno yanavyoongelewa mitaani.
Akiongea katika kipindi cha The playlist cha Times Fm Jumamosi iliyopita, Rapa huyo ameshangazwa na maneno hayo ambayo amedai hajui yanatokea wapi.

“Sijui haya maneno yanatokea watu, ni vitu ambavyo watu wanatumia kwa siri sana ila mimi sijawahi kumuona TID akitumia, na tunasafiri kila kwenda sehemu kibao hata dalili za mtu anayetumia madawa ya kulevya sijawahi kuziona kwa TID.

“Sijui sijawahi kumuona kwa kweli” alisema

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.