Picha za Mrembo Anayedaiwa Kutoka Kimapenzi na Diamond Platnumz, Timu Zari Waendelea Kumuandama - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Picha za Mrembo Anayedaiwa Kutoka Kimapenzi na Diamond Platnumz, Timu Zari Waendelea Kumuandama


Mashabiki wa Zari the Bosslady wanamshambulia Lynn, mrembo aliyetumika kwenye video ya ‘Kwetu’ ya msanii wa WCB, Raymond kwasababu wamesikia tetesi kuwa amechepuka na Diamond Platnumz.

Tetesi hizi ni kubwa kiasi ambacho watu walio karibu na mastaa hao wamedai kuwa zimeitikisa ikulu ya Chibu. Wanadai kuwa Zari amekerwa na tetesi hizo na kwamba uhusiano wao umepata dosari.

Wiki hii tetesi hizo zimevuma zaidi kiasi ambacho mashabiki wa Zari wamekuwa wakimmiminia matusi Lynn kwenye akaunti yake ya Instagram.

Inafurahisha kwasababu Lynn haoneshi kutikiswa na matusi hayo huku pia akipewa support kubwa kutoka kwa mashabiki ambao hawampendi Zari. Of Course Team Wema yote inaonesha kuwa nyuma yake!

Cha kuvutia zaidi ni kuwa Lynn ni msichana mdogo na mrembo sana kiasi ambacho wasiompenda Zari wanasema anafaa zaidi kuwa kifaa cha Bin Mondi. Kwa wengi hizi bado ni tetesi tu lakini kama ukiangalia post za nyuma za Lynn, utagundua kuwa alikuwa shabiki mkubwa wa Daimond kwakuwa amekuwa akiweka picha zake [Diamond] mara kwa mara.Nini Maoni Yako Kuhusu Hii ?

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.