Nuh Mziwanda Amwagana na Mpenzi Wake Mpya..Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nuh Mziwanda Amwagana na Mpenzi Wake Mpya..Ipo Hapa

MKALI wa Bongo Fleva, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amefunguka kuwa, amemmwaga mpenzi wake aitwaye Erah Erah licha ya kwamba penzi lao lilitawaliwa na mbwembwe nyingi.

Akipiga stori na paparazi wetu kuhusiana na maendeleo ya penzi lao, Nuh alifunguka kuwa demu huyo haikuwa riziki kwake kwani hakudumu naye baada ya kugundua hamfai na penzi lao limedumu kwa wiki mbili tu.

“Yule nimeshatemana naye, nitampata mkali zaidi yake,” alisema Nuh na kuongeza:

“Nilikuwa na Shilole, nikamuacha, nikampata Erah ambaye naye nimemuacha, naamini nitampata mkali zaidi yao.”

Nuh na Shilole walimwagana hivi karibuni huku kila mmoja akidai hakuwa na amani kwenye uhusiano huo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.