Niko tayari kuolewa na Wizkid - Lulu la Diva - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Niko tayari kuolewa na Wizkid - Lulu la Diva

Msanii wa kike ambaye pia ni muuza nyago katika Video za Kibongo, Lulu Abbasi ‘Lulu La Diva’ amefunguka kuwa yuko tayari kuolewa na msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun ‘Wizkid’. Akizungumza na Global TV Online hivi karibuni, Lulu alisema yuko tayari kufanya mambo mengi sana na Wizkid hata kama ni kumuoa.

“Niko tayari kufanya naye kazi na nitafanya naye ikitokea hivyo na nitafanya naye vitu vingi sana hata kama akitaka kunioa niko tayari,” alisema Lulu La DIVA. Lulu La Diva ameuza nyago katika video ya Wimbo wa Naogopa wa Mirror na Baraka Da Prince.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.