Nikki wa Pili awatetea wanawake wa Kichaga - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nikki wa Pili awatetea wanawake wa Kichaga

post-feature-image
Baada ya kutamba na wimbo wa ‘Baba Swalehe’ mkali wa Bongo Fleva, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’, anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa ‘Sweet Mangi’.

 Katika wimbo huo aliomshirikisha Chidy Benzi, anayepatiwa matibabu baada ya kutumia dawa za kulevya, Nikki kutoka kundi la Weusi amezungumzia kabila la Wachaga kwamba ni wazuri na wanajua kupenda.

“Wengi wanasema wasichana wa Kichaga hawajui kupenda wanawaza fedha, lakini ukisikiliza wimbo wangu utajua namna wanavyopenda kuliko wanavyofikiriwa na wengi,” alisema Nikki.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.