Nay Awasihi Mastaa Kukaguliwa Silaha - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nay Awasihi Mastaa Kukaguliwa Silaha

EMMANUEL Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amewataka mastaa wenzake kujitokeza haraka kuhakiki silaha zao ili kutii agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alilolitoa hivi karibuni.
Nay anayefanya poa kwenye gemu la Bongo Fleva, amesema kutambua umuhimu wa kukaguliwa, aliipeleka bastola yake mapema kukaguliwa ikiwa ni siku moja mara baada ya Rais John Pombe Magufuli silala zake kukaguliwa.
“Hakuna sababu ya kusubiri siku zipite halafu watumbuliwe. Kila mtu amesikia agizo ni bora kutekeleza, nawasihi ambao hawajafanya hivyo wafanye maana watafikiwa na mkono wa sheria,” alisema Nay.
Machi 18, mwaka huu Makonda alitoa agizo la wakazi wote wa Jiji la Dar kuhakiki silaha zao kuanzia Aprili Mosi hadi Julai Mosi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.