Msanii Wa Yamoto Band,Aslay Aongelea Kwanini Hayuko Tena na Mwanamke Aliyezaa Naye - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Msanii Wa Yamoto Band,Aslay Aongelea Kwanini Hayuko Tena na Mwanamke Aliyezaa Naye

Bet Sasa
Aslay ni mwimbaji kutokea kundi la Yamoto BAND, kilichofanya awepo kwenye hii post ni kauli yake ya kukanusha kumtelekeza Mwanamke mwenye ujauzito wake baada ya kuishi nae kwa miezi isiyozidi 6.
Aslay ambaye ana umri wa miaka 20 sasa hivi amesema ‘Baada ya kuishi pamoja miezi sita tulizinguana ikabidi kila mtu ashike hamsini zake, sisi vijana bwana mambo mengi… tukaangalia pia mimi bado umri wa kukaa na Mwanamke na yeye akaona bado umri wake wa kukaa na Mwanaume
aslay 3
Aslay na mzazi mwenzie
Sikuchukua uamuzi ila wote ndio tulichukua uamuzi…. nilimuacha na ujauzito wangu na tayari amejifungua mtoto wa kike ambaye ana kama mwezi mmoja na nusu, mwanangu nimemuita Moza jina la marehemu mama yangu… na bado mpaka sasa tunaonana hata hapa nimetoka kumuona mwanangu, hatujarudiana…. tunashirikiana tu kama mtu na mzazi mwenzake‘ – Aslay
Kingine alichokiongea Aslay kwa sasa ni kwamba amekabidhiwa majukumu mapya ya kuwa meneja, aliyemkabidhi ni boss wake Mkubwa Fela kiongozi wa Mkubwa na Wanawe na sasa Aslay ni meneja wa madada watano aliokabidhiwa miezi mitatu iliyopita na watasikika very soon.
Unaweza kumtazama Aslay hapa chini..

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.