Mr Blue na Alikiba Kuja na Bonge La Mkwaju Soon. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mr Blue na Alikiba Kuja na Bonge La Mkwaju Soon.

Bet Sasa
Nyota wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr Blue’ ambaye hivi karibuni aliuaga ukapera kwa kuamua kufunga pingu za maisha na mzazi mwenzake, Wayda, amedai anatarajia kuachia wimbo mpya ambao amemshirikisha Ali Kiba.

Mr Blue amedai kwamba wimbo huo utajulikana kwa jina la ‘Mboga Saba’

Akizungumza na MTANZANIA, Mr Blue alisema kuwa wimbo huo upo tayari na anatarajia kuuachia wiki ijayo endapo mtayarishaji wake, Man Water atamkabidhi.

“Kiukweli huu wimbo haujawahi kutokea na utakuwa bonge la wimbo kwa kuwa tumekutana wakali wa muziki, ninaamini wimbo huo utakuwa ni historia katika tasnia ya muziki hapa nchini,” alisema Mr Blue.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.