Matumizi Ya Madawa Ya Kulevya Yatatufanya Tushindwe Kuaminika Na Jamii – AY - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Matumizi Ya Madawa Ya Kulevya Yatatufanya Tushindwe Kuaminika Na Jamii – AY

Bet Sasa


Ambwene Yessaya ‘AY’, amesema kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini kutashusha soko la wasanii hao kwa kukosa uaminifu.


Akizungumza na gazeti la Mtanzania Alhamisi hii, AY amesema hizi kashfa za wasanii kutumia madawa ya kulevya inawachafua wasanii.
“Mimi binafsi nashindwa kuelewa kwanini wasanii wanajitumbukiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na huko tunakoelekea tutashindwa kuaminika kwa jamii, familia zetu hata kwa watoto na marafiki, inabidi tupigane kwa pamoja, huku tukimshirikisha Mungu atuepushe na hayo mambo,” alisema AY.
AY aliongeza kwa kuwa muziki wa kizazi kipya kwa sasa una nafasi kubwa, wasanii watumie fursa hiyo kujiendeleza kimuziki kwa kushirikiana na wasanii wa mataifa mbalimbali, ili kukuza uchumi badala ya kushirikiana katika matumizi ya dawa za kulevya.
“Kinachotakiwa kwa sasa, wasanii watumie fursa za kushirikiana na wasanii wenye mashabki wengi kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kujiongezea mtandao, soko na fedha zaidi, siyo kujiingiza katika matumizi au uuzaji wa dawa za kulevya,’’ alifafanua AY.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.