Man United, Liverpool, West Ham Zaibuka Kidedea Ligi Kuu Ya England - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Man United, Liverpool, West Ham Zaibuka Kidedea Ligi Kuu Ya England

Ligi kuu England iliendelea usiku wa Jumatano 20 April kwa michezo mitatu kupigwa huku timu za West Ham, Liverpool,Man United wakishinda michezo yao. Wagonga nyundo wa West Ham wameibuka na ushindi wa maboa 3-1 dhidi ya Watford, mshambuliaji Andy Carrol, akifunga goli la kwanza dakika ya 11 kisha kiungo Mark Noble akifunga mabao mengine mawili kwa mikwaju ya penati.
Liverpool wakashinda dabi yao kwa kuwachapa Everton kwa mabao 4-0, mabao ya majogoo hao yakifungwa na Divock Origi, Mamadou Sakho,Daniel Sturridge,Philippe Coutinho.

Nao Man United wakaibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace, beki Damien Delaney alianza kuipa Man United goli la kuongoza baada ya kujifunga kisha beki wa kiitaliano Matteo Darmian akaongeza bao la pili na kuipa timu yake alama tatu muhimu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.