Lady Jaydee akutana na Ray C, amwandikia ujumbe huu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lady Jaydee akutana na Ray C, amwandikia ujumbe huu

Msanii wa muziki, Lady Jaydee amekutana na Ray C hivi karibuni na kumshauri mambo kadhaa kuhusu afya yake.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa Ndindindi, ameonyesha kutoridhika na afya ya Ray C na kuamua kumwandikia ujumbe wa kumpa matuamaini.
Kupitia instagram, Jay Dee ameandika:

A message of Hope: Kila mtu anapitia magumu katika maisha kwa njia tofauti hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea. Amini na amua nakupa moyo na Mungu akusaidie kwa yote unayopitia akuondolee akuepushie na akupe kufahamu na kukiri mabaya.
Watu wanakupenda nakumbuka tulivyoanza kimtindo nai miss competition pls Come Back naamini bado unayo nafasi . Binti amka jikaze anza mwendo, umrembo na bado wang’ara . Ni baada ya miaka 6 tangu kuonana mara ya mwisho, story nazo ni ndefu na nyingi
Ombi:
Tuheshimu na kuhurumia matatizo ya wengine, tafadhali msi comment vibaya wala kwa kejeli.
Lolote linaweza kumfika yoyote
Saa yoyote
Tuonyeshe Mapenzi
#PowerOfPositivity

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.