Kumbe Davido Ni Mvuta Bangi, Cheki Alivyonaswa Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kumbe Davido Ni Mvuta Bangi, Cheki Alivyonaswa Hapa

Ishu ya siku nyingi dhidi ya mwanamuziki kijana wa Nigeria, Davido, kutumia madawa ya kulevya, yalizidi kujidhihirisha hivi majuzi alipokutwa akivuta bangi studio. Wafutatiliaji wa jambo hilo wanasema ni sababu hiyo iliyojenga uhasama kati ya mwanamuziki huyo na mzazi mwenzake, Sophie, ambaye alifanya juu chini kumchukua mwanaye mdogo kwa kuogopa kuhusishwa na madawa hayo.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Davido alidaiwa kupromoti madawa ya kulevya katika video yake iitwayo ‘Fans Mi’ ambayo alimshirikisha rapa wa Marekani, Meek Mill. Jambo hilo limemfanya Mkurugenzi wa Masuala ya Jamii ya Nigeria (NDLEA), Mitchell Ofoyeju, kusema kikosi cha kupambana na madawa hayo kimeunda jopo la kuichambua video hiyo.

Hata hivyo, meneja wa Davido, akijibu tuhuma hizo majuzi alisema: “Watu wamekuwa wakizungumzia suala hilo katika vyombo vya habari. Huenda wanahitaji muda zaidi kuitazama video hiyo tena na kuona inamaanisha nini. Sijui ni kwa nini mtu adai kwamba Davido anajihusisha na madawa ya kulevya! Unga wa viazi ulielezewa vyema katika video hiyo, kwani ulionyeshwa hadi unga huo unavyopikwa na kuliwa na mchuzi wa mboga.”

Hata hivyo, wafuatiliaji wanasema, kilichotokea wakati huu si unga wa viazi bali kitu kinachoweza kumtosa mtu gerezani akikutwa nacho.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.