Jaguar: Nilijaribu Kumsaidia Chidi Benz, Tatizo Hupoteza Matumaini Mapema - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jaguar: Nilijaribu Kumsaidia Chidi Benz, Tatizo Hupoteza Matumaini Mapema

Staa wa Kenya, Jaguar amedai kuwa amewahi kujaribu kumsaidia Chidi Benz aondokane na matumizi ya madawa ya kulevya lakini ilikuwa ngumu kwasababu rapper huyo hupoteza matumaini mapema. 12558535_975354382558641_14786179_n
Akiongea kwenye kipindi cha Mseto cha Radio Citizen, Jaguar alisema Chidi amekuwa akidai kuwa muziki wake hauchezwi redioni, jambo linalomchanganya na kumfanya aendelee kutumia unga.
“Chidi Benz nimeongea naye kwa muda mrefu hata nilienda TZ na kuna picha kwenye mtandao tuko naye. Kibaya kuna watu unaweza ukawasaidia na wengine usiwasaidie, mfano kama Chidi ni rafiki yangu ukiongea naye analose hope haraka sana na maisha,” alisema Jaguar.
“Kama sasa ananiambia kuna watu walikataa kucheza muziki wake, mimi tunakaa chini na AY tunaongea, tunamuambia wewe ingia studio AY atasimamia lakini unapata analose hope haraka sana. Sasa huwezi ukafanya kila kitu kwa mtu,” aliongeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.