Hii ni sababu kwanini wimbo wa Rama Dee ‘Kipenda Roho’ umewarudisha karibu Idris na Wema - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hii ni sababu kwanini wimbo wa Rama Dee ‘Kipenda Roho’ umewarudisha karibu Idris na Wema

Bet Sasa
Nyimbo zilizoandikwa kwa ustadi, kuimbwa kwa hisia, zenye sauti tamu na kunakishwa na ala za muziki maridhawa, zina nguvu ya kufanya mambo makubwa yasiyofikiriwa.
Na hicho ndicho wimbo mpya wa Rama Dee, Kipenda Roho umefanya maajabu katika maisha ya Idris Sultan. Wajua jinsi ambavyo hivi karibuni moyo wa Idris ulivunjwa na mpenzi wake Wema Sepetu kwa kusambaa video inayomuonesha akimbusu mwanaume mwingine.
Kipenda Roho umebeba ujumbe mzito unaokisi hisia za moyo wa mshindi huyo wa Big Brother Africa 2014. Na kwakweli ni wimbo unaomgusa kila mmoja anayejua maana ya kupenda. Ni wimbo uliomfanya staa huyo aliyejaa vituko, aufungue moyo wake na pengine kufikiria mara mbili umuhimu wa kulipa nafasi ya pili pendo lake kwa Wema licha ya yote yaliyotokea.
“Rama Dee Kipenda Roho aiseeee hii nyimbo ni habari nyingine unaweza mrudia ex wako wa 1970 wakati umezaliwa 80,” ametweet Idris.
Aliongeza kwa kumjibu Rama Dee: @RamaDee3 Bro mpaka Wema ameni-unblock.”
Hakuishia hapo, alipost kipande cha video Instagram akicheza wimbo huo na kuandika: Tag people you love the most ❣ kanatia chozi haka kanyimbo.”Kwa upande wake Rama Dee ameiambia Bongo5: Kwanza jamaa mkweli sana…ameweza kuonyesha kitu ambacho kimemuingia hilo ni kubwa na tofauti sana kwa watu wengi haswa sisi vijana wa miaka 80-87. Wimbo huu hata mimi mwenyewe huwa unanipotezea muda kama nikibonyeza play.”


“Mwanga umefanya watu waone, wakosoe ni sumu tuu, chombo kwenye maji lake jua yake mvua safari tu, kwenye mvua matope samdumba ohoo, isikufanye uchoke mchumba ohoo wanapanga maneno kama chati za kumi bora. Kupima upendo ni hatari, mbele tu naaaaona vita, kipenda roho roho yangu nishike mkono kuyapita kipenda roho roho yangu, tulishinde lengo lao lao,” anaimba Rama Dee.
Amesema kwa sasa anafanya mipango ya video yake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.