HabariNjema: Gardner G. Habash Arudi CloudsFM...Jionee Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

HabariNjema: Gardner G. Habash Arudi CloudsFM...Jionee Hapa

Bet Sasa
Gadna 2
Gardner akisaini mkataba wake mpya pembeni ya mkuu wa vipindi CloudsFM Shaffih Dauda
Ni miongoni mwa Watangazaji wenye majina makubwa na waliofanya vizuri sana kupitia CloudsFM, Radio yenye zaidi ya miaka 16 toka ianze kurusha matangazo yake kwenye sehemu mbalimbali Tanzania.
Kabla ya kutangaza kuacha kazi CloudsFM December 2010, Gardner aling’aa sana kupitia show za JAHAZI na hata CloudsFM Top 20 miaka hiyo na sasa habari kubwa na nzuri kwa mashabiki wote wa CloudsFM ni kwamba Gardner G. Habash a.k.a Captain amerejea CloudsFM na ameshasaini mkataba.
Gardner anarudi kui-run show ileile aliyoiacha wakati anaondoka, JAHAZI CloudsFM time hizo akiwa na Ephraim Kibonde na sasa wataendelea kuwa pamoja kuanzia saa kumi jioni mpaka saa moja usiku ambapo Gardner amefanya Exclusive Interview na Zamaradi Mketema wa TAKE ONE CloudsTV na itaonekana leo usiku so kuanzia saa tatu kaa karibu na TV yako.
Kwenye Interview yake na MKASI TV October 2014Gardner G. Habash alisema ‘nimeifanyia mambo mazuri bongofleva na ningependa kutumwa zaidi kufanya mambo mazuri, kingine kizuri zaidi kwenye show zangu napiga sana nyimbo za bongofleva kuliko nyimbo za kutoka sehemu nyingine’
Kuhusu historia yake ya kuanza kazi ya utangazaji, Gardner G aliiambia MKASI TV kwamba aliingia CloudsFM kama mtu wa masoko na ni baada ya kuchukuliwa na mteja wake aitwae Othman Njaidi ambaye alikua anamkubali Gardner sababu alikua na uwezo wa kumshawishi mteja yeyote kununua chochote kwani wakati huo Captain G alikua akiuza kanda za video na audio Mwanza.
‘Nilimwambia Othman Njaidi ninahamu ya kufanya kazi kwenye Radio akanichukua mpaka CloudsFM na kunikutanisha na Ruge nikafanye kazi kwenye timu ya watu wa masoko na sio mtangazaji lakini nilipokutanishwa na Ruge Mutahaba aliponisikia lafudhi yangu akasema huyu anafaa kuwa Mtangazaji, akanipeleka kipindi cha AFRIKA BAMBATAA na Marehemu Amina Chifupa na kuanzia hapo ikabaki historia’ – Gardner
Una chochote cha moyoni kuhusu kurudi kwa Captain G CloudsFM ? unaweza kuniachia comment yako hapa chini mtu wa nguvu.
-millardayo

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.