Diamond Akitaka Kuandika Wimbo Wa Kuumizwa Kimapenzi Humfikiria Msichana Huyu (Audio) - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Akitaka Kuandika Wimbo Wa Kuumizwa Kimapenzi Humfikiria Msichana Huyu (Audio)

Diamond Platnumz ni bingwa wa kuandika nyimbo za kuachwa, kuumizwa na kutendwa kimapenzi.
Kamwambie, Mbagala, Mawazo, Ukimwona, Nataka Kulewa, Bado na zingine, zilihit kwasababu ziligusa maisha ya wanaume wengine wahanga wa malavidavi. Lakini staa huyo ambaye hivi karibuni alisema Zari ameutunza moyo wake kwenye friji kiasi cha masuala ya kuumizwa kuyasikia tu kwa wengine kwa sasa, humkumbuka msichana mmoja kila anapotaka kuandika nyimbo za aina hiyo.
Si Wema wale ex wake mwingine unayemfahamu, Harmonize amemtaja baada ya mimi kumuuliza tetesi kuwa mashairi ya bosi wake huyo kwenye Bado, yalimlenga ex wake, Wema Sepetu.
“Diamond hajaanza kuimba leo mambo ya kuachwa, aliimba Kamwambie, akaimba Mbagala,” Harmonize amesema kwenye Chill na Sky.
“Mimi naamini kabisa, hata mimi mwenyewe nilivyomuuliza ‘kwani ulimuimbia nani Kamwambie?’ akasema mimi nikitaka kuandika nyimbo yoyote ya mapenzi namkumbuka Sarah mwanamke ambaye nilimpenda sana.”
Sikiliza Chill na Sky na Harmonize hapo chini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.