Clouds Fm Yawapa Shavu Watangazaji Wa East Africa Radio....... - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Clouds Fm Yawapa Shavu Watangazaji Wa East Africa Radio.......


Ile Vuta N’kuvute ya vituo vya redio inaendelea na sasa East Africa Radio imekuwa mhanga mpya.

Dj wa kike, Sinyorita na mtangazaji wa The Cruise, Mami wanadaiwa kuondoka East Africa Radio kuanzia wiki hii baada ya kupata dau kubwa kutoka kwa guess what? Clouds FM.

Tetesi hizo zilianza kuvuma tangu wiki iliyopita lakini jana zimeonekana kupata ukweli baada ya wawili hao kutosikika kwenye kipindi cha The Cruise, kitu ambacho si cha kawaida.

Tetesi zinadai kuwa tangu Dj Fetty aache kazi Clouds FM, wamekuwa wakitafuta mtangazaji wa kike anayeweza kuchukua nafasi yake na Mami anaonesha kuwa na caliber hiyo.

Tayari wawili hao wamebadilisha profile zao za Instagram kwa kuondoa kipengele cha kuwa ni wafanyakazi wa East Africa Radio.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.