Belle 9 Kuja na ‘remix’ ya Burger Movie Selfie - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Belle 9 Kuja na ‘remix’ ya Burger Movie Selfie

STAA wa Bongo Fleva, Abednego Damian ‘Belle 9’ hivi karibuni anatarajia kuachia ‘remix’ ya wimbo wake unaotamba kwa sasa kwenye gemu uitwao Burger Movie Selfie huku akisema utasheheni mastaa wengi wa muziki waliokubali kumpa ‘sapoti’.

Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Belle 9 alisema kwa kipindi kirefu tangu ajikite kwenye ulimwengu wa muziki katika ngoma zake zote alizowahi kuzitoa hakuna yenye sifa ya kuirudia licha ya mashabikia kumlilia kufanya hivyo, ila hii ameamua kuirudia kwa kuwa inastahili.

“Unajua wimbo wangu unafanya vizuri sana kwa sasa kwenye gemu ni wimbo ambao bado watu wanapenda kuendelea kuusikiliza kwa hiyo ili kuuboresha nimeamua kuufanyia remix nitakayoiachia hivi karibuni kwa kuwashirikisha baadhi ya mastaa ambao siko tayari kuwataja majina yao kwa sasa,” alisema Belle 9. 

-GPL
Download App Yetu  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Time BURE Kabisa !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.