Babu Tale Aeleza Alivyosaidiwa Na Ray C Kipindi Hajulikani - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Babu Tale Aeleza Alivyosaidiwa Na Ray C Kipindi Hajulikani
Babu-Tale


 Meneja wa Tip Top Connection na WCB, Babu Tale, amefunguka kuwa anatamani kumsaidia Ray C kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya na kumrejesha vizuri kwenye muziki kama zamani kwakuwa naye aliwahi kumsaidia.

Akiongea kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM, Jumamosi iliyopita, Tale alidai watu wengi hawajui Ray C alimsaidia kwa kiasi kikubwa kukaa kwenye ramani nzuri kisanaa kama alivyo leo.


“Natamani sana kumsaidia Ray C, natamani mno, zamani nilikuwa naigiza sauti za watu hata mia, ikaenda kipindi hicho Ray C anafanya kazi East Africa nilikuwa nafanya naye mi kazi yangu ilikuwa kugeza sauti, wakina mzee Msekwa nini,” alisema Tale.
“Na mimi ndiyo nilimchukua Babu Ayubu, sikuwahi isema hii, sijaonana naye ila nimepanga ndani ya siku hizi mbili nione namna ya kumsaidia,”aliongeza.
Tale aliongeza kuwa imefika wakati Tanzania kijengwe kituo maalum (rehab) kwaajili ya watu maarufu ambacho wasanii na watu maarufu wengine watakuwa hawachanganywi na watu wa kawaida.
-Bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.