Aunt Ezekiel Atumbuliwa Jipu Na Serikali Ya Magufuli, Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Aunt Ezekiel Atumbuliwa Jipu Na Serikali Ya Magufuli, Ipo Hapa

Kaulimbiu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ‘JPM’ ya kutumbua majipu na watu wasiolipa kodi imemdondokea staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson baada ya gari lake aina ya Audi kukamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa tuhuma za kuingizwa nchini kinyemela bila kulipiwa ushuru na kukwepa kodi.

Habari kutoka kwa vyanzo vya kuaminika zilieleza kuwa tukio la Aunt kutumbuliwa lilijiri hivi karibuni ambapo staa huyo alikuwa akificha siri hiyo isinaswe na mapaparazi wetu, jambo ambalo limemshinda.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Wikienda lilimsaka Aunt kutaka kujua kisa kamili ambapo alipobanwa alikiri kukamatwa kwa gari lake hilo kwa makosa ya kukwepa kodi wakati linaingizwa Bongo hivyo kuwa mikononi mwa TRA.

“Kweli gari langu limeshikiliwa na TRA ila haina tatizo sana kwani wamekagua, karibia kila kitu kipo sawa isipokuwa ninadaiwa kodi tu ambayo nayo si fedha nyingi kiasi cha kunishinda. Waliniambia vibali vyake vyote viko sawa na kwamba lipo nchini kihalali kabisa hivyo ninachotakiwa kulipia ni kodi tu ambayo najipanga kulipia muda wowote.
“Nilishtuka sana baada ya kukamatwa kwani nilihisi ndiyo mwisho wa kuwa na gari langu lakini sasa nimepata moyo baada ya kuambiwa hakuna kilichochakachuliwa.

“Natafuta Sh. milioni 10 na kitu ili niweze kulikomboa,” alisema Aunt aliyedai gari hilo alinunuliwa na baba mtoto wake, Moses Iyobo ‘Moze’ huku akigoma kutaja bei yake.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.