Atletico Madrid Yaihadhibu Barcelona UEFA. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Atletico Madrid Yaihadhibu Barcelona UEFA.

Wachezaji wa Atletico Madrid wakishangilia ushindi dhidi ya Barcelona

Mabingwa watetezi Barcelona walipata mshtuko kwa kutolewa Ligi ya Mabingwa baada ya Antoine Griezmann kufunga magoli mawili na kuipeleka Atletico Madrid nusu fainali.

Barca iliwasili katika mji mkuu wa Hispania wakiwa wanaongoza 2-1 kutoka kwenye mechi ya kwanza lakini ulinzi duni ulimfanya Griezmann kuwatoa mashindanoni.
Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone

Nao Bayern Munich iliweza kufudhu nusu fainali baada ya kutoka suluhu ya 2-2 (3-2) dhidi ya Benfica ya Ureno.

Magoli ya Benfica yalifungwa na Jimenez Rodriguez na Souza Conceicao huku ya Bayern Munich yakifungwa na Arturo Vidal na Thomas Muller.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.