Ali Kiba aeleza jinsi ‘alivyommiss’ dada yake Diamond, Queen Darleen - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ali Kiba aeleza jinsi ‘alivyommiss’ dada yake Diamond, Queen Darleen

Bet Sasa
Msanii wa muziki Alikiba amefunguka kwa kusema kuwa kuna wakati huwa anamkumbuka sana msanii wa kike ambaye ni dada wa msanii Diamond Platnumz, Queen Darleen.
Ali Kiba na Darleen walikuwa washkaji zamani, ambapo Queen Darleen aliwahi mshirikisha Ali Kiba katika wimbo wake, ‘Wajua’ ambao ulifanya vizuri sana.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatatu hii, Ali Kiba alifunguka kwa kusema yeye mwenyewe anamkumbuka Queen Darleen sababu kuna vitu walikuwa wanaendana.
“Queen Darleen alikuwa mkongwe katika gemu na tulikuwa na ukaribu sana,” alisema Ali Kiba. “Kiukweli muda mwingi huwa nina ‘M-miss’ sababu mimi na yeye kuna vitu vingi tulikuwa tukiendana kama washikaji. Muda mwingine akili yangu na yake ni kama sawa vile”,
Kwa sasa wawili hao hawaelewani huku watu wakidai hali hiyo imesababishwa na ugomvi uliopo kati ya Diamond na Ali Kiba.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.