AJABU: Mwanafunzi wa kiume apata ‘Hedhi’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

AJABU: Mwanafunzi wa kiume apata ‘Hedhi’


Dunia ina mambo waswahili hawakukosea kusema hili, kila kukicha linaibuka jipya ambalo kwa namna moja ama nyingine linaweza kukuacha mdomo wazi.
Umeshawahi kukutana na mwanaume ambaye hupata siku za mwezi kama kawaida kama wapatavyo wanawake?

Nakukutanisha na George Fellowes ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 22 na anaamini kwamba hata yeye hupatwa na ‘hedhi ya kiume’.

Anasema kuwa ni rafiki wa karibu wa Amber May Ellis jirani yake na hivyobasi hupata uchungu wa hedhi kila mwezi rafikiye anapopata hedhi.

Uchungu huo anasema huwa mkali hadi kulazimika kuchukua likizo ya kuwa mgonjwa.

Akizungumza na Newsbeat George alisema:Nadhani ni swala la kifikra kwa sababu sisi ni marafiki wa karibu sana na tuna hisia sawa.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliopita anasema kuwa amekuwa akipata uchungu wa hedhi na ishara hizo ni sawa na zile za wanawake.

“Ninapata uchungu chini ya tumbo langu pamoja na katika kinena.Huwa nahisi vibaya na kuwa na hasira na marafiki wangu wengi. Pia huwa na hisia zenye mhemuko,” alisema.

George anaelezea kwamba wakati alipoanza kupata uchungu miaka mitatu iliopita alitaka ushauri wa daktari wake. Lakini hakukuwa na maelezo hivyo basi alipewa dawa za kumaliza maumivu ya kinena.

-BBC

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.