Wimbo wa ‘My Life’ Ulivyoyagusa Maisha ya Dogo Janja - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wimbo wa ‘My Life’ Ulivyoyagusa Maisha ya Dogo Janja

Muziki ni sanaa ambayo watu wanaweza kujifunza kupitia mashairi yake. Inaweza kikawa ni kitu ambacho kiliwahi kutokea au hakijatokea pia.
Kwa sasa ‘My Life’ ambao ni wimbo wa Dogo Janja unafanya vizuri. Watu wamevutiwa zaidi na jinsi msanii huyo alivyobadilika kwenye style ya kuimba japo kuna sehemu ametumia style yake ya mwanzo.

Dogo Janja ameweza kutumia mashairi ambayo mengine ndani yake yameweza kumgusa moja kwa moja kwenye maisha yake halisi.

“Kitambo mimi nachana zaidi hata ya wanyamwezi”, ukiangalia wakati Dogo Janja ametoka na nyimbo zake za kwanza alikuwa na umri mdogo sana na style yake iliwavutia mashabiki kibao, wakati huo huo alimkuta Young Dee peke yake akiwa ni msanii mwenye umri mdogo kwa kipindi hiko. Kipindi hiko Dogo Janja aliweza kushika vizuri na kufanya show kibao.

“Kurap mimi ni mkali, staili na mitindo. Muulize Hamadi Ally alivyonikutaga chimbo”, Ni kweli Madee alimkuta Dogo Janja Arusha ambako ndiko chimbo alilolitaja kwenye nyimbo hiyo. Hata ukimuuliza leo Madee atakubali kuwa Dogo Janja ni mmoja kati ya wasanii wenye kipaji ambao amewahi kukutana nao ndio maana akaamua kumchukua kutoka Arusha hadi Dar na kukaa naye.

“Msomi Nick wa Pili, mimi niliachaga Makongo”, Dogo Janja ameongeza idadi ya wasanii wa bongo waliokimbia shule baada ya kuishia kidato cha pili, hali ilikuwa ngumu pale matokeo yalipotoka vibaya ya mtihani wa taifa akatakiwa arudie tena darasa hilo hilo. Amemtaja Nick wa Pili ni mmoja kati ya wasanii wachache wasomi hapa bongo ambaye kwa sasa anasoma Udsm akitafuta Phd lakini bado anaendelea kufanya mziki.

Hongera kwa Dogo Janja kwa wimbo huo mzuri ambao umeonesha jinsi gani ulivyokua. Endelea kutoa vitu vizuri nafasi yako bado ipo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.