Waziri Mkuu Majaliwa Amsimamisha Kazi Daktari Kwa Kuomba Rushwa ya Laki Moja. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Waziri Mkuu Majaliwa Amsimamisha Kazi Daktari Kwa Kuomba Rushwa ya Laki Moja.

Siku ya jana 29, February Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimsimamisha kazi mmoja wa Madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Wilaya mkoani Mtwara.

Daktari huyo alituhumiwa kuomba rushwa ya Shilingi laki moja kutoka kwa mgonjwa, hatua hiyo ikampelekea pia Waziri Mkuu huyo kukasirishwa na kuagiza maduka yote ya dawa yaliyokaribu na hospitali hiyo kufungwa mara moja kutokana na madaktari kujihusisha na biashara hiyo na kuachana na dawa za Serikali.

Maneno ya Mh. Kassim Majaliwa;

‘Nani alitaka laki moja kutoka kwa mgonjwa?, simama mwenyewe.. ulimuambia kanunue dawa, dawa shilingi 80 unasema kanunue alafu leta laki moja, ameleta dawa unamwambia laki moja yangu iko wapi?’

‘Sasa naanza na wewe, unasimama kazi na uchunguzi uendelee, na wengine wote ntakao wabaini basi utaratibu ni huu‘

-millardayo

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.