Vijana Ni Wakati Wa Kuwa Original. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Vijana Ni Wakati Wa Kuwa Original.

Bet Sasa
Inasemkana kwamba, “ni bora kushindwa katika kuwa Original kuliko kifanikiwa kwa kuiga”. Kwa bidhaa ya kondomu halisi na kongwe za kitanzania, Salama kondomu imeibuka na msemo wa “Kuwa Original” kwa ajili ya vijana. Kuwahamasisha kukubaliana na kusherehekea uhalisia wao !
Sasa, unaweza kusema “ni rahisi kutamka kuliko kutenda” ukizingatia jinsi vijana walivyo leo hii katika jamii. Kila mtu anataka kuwa mtu fulani na kila mmoja anataka mafanikio. Lakini siku zote kuna matumaini kwa wale ambao wanajitahidi/wanaopambana kuwa wajasiri na tofauti. Na kwa hilo akilini, Salama kondomu wamechukua hatua ya kuwatafuta vijana wajasiri na Original watakaosimulia hadithi zao.
Kuna wasanii wengi vijana siku hizi. Wengine hupenda kushuka mistari vyumbani mwao, baadhi katika studio gizani chini kwa chini Ubungo, bila kitu chochote bali midundo. Pia kuna baadhi yao wanapendelea kuwa katika mkumbo wa wapenzi na marafiki kuwasikiliza wakishuka misatari kama Faraji Junior, kijana wa Kitanzania akiwa ni rapa na mtunzi ambaye ni sehemu ya kundi hilo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.