Uaminifu Nguzo Muhimu Katika Mahusiano. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Uaminifu Nguzo Muhimu Katika Mahusiano.


By Danieller Kitimbo

Katika maisha  ya  mwanadamu  kitu  cha  muhimu  ni  upendo. Upatapo  mtu  anayekupenda  na  kukuthamini  na  kukuelewa  maisha  yako  huwa  yanabadilika  hata  mwonekano  wa  nje  wa  mtu  huwa  unabadilika.

Jambo  la  msingi  katika  maisha  ya  mwanadamu  ni  uaminifu. Haswa  kwenye  maswala  ya  mahusiano;mahusiano  yanapo  kuwa  na  upendo  ila  bila  uaminifu  ni  kazi  sana  kudumu.Uaminifu  ndio  nguzo moja  wapo  kuu  nayo  beba  mapenzi  baina  ya  watu  wa  wawili  ambao  wanapendana.
Uaminifu  sio  swala  tu  la  kuwa  na  mpenzi  moja, bali   uaminifu    inahusisha  kuwa  wawazi  juu  ya  jambo  Fulani  linalohusiana  na  maisha  yenu  wote   wawili.wengi  hufikiri  uaminifu  ni  swala  la  kuwa  na  mpenzi  moja  la  hasha  sio  kweli.Bali  uaminifu  ni  kitendo  cha uwezo  wa  kuuliza  kitu   pale  uonapo  jambo  haliko  sahihi  na  unashindwa  kuelewa.
Kukosekana  kwa  uaminifu  kunaleta  kugombana  kutokuaminiana  na  pia  mwisho  huleta  kuvunjika  kwa  mahusiano  ambayo  hugharimu  muda  mwingi  sana  wa  mtu  mpaka  hapo   atakapo  kuja   kukaa  sawa  na  kurudi  katika  maisha  yake  ya  kawaida,na  mara  nyingine  humfanya  mtu  kuwa  mwoga  sana katika  kuanzisha  mahusiano  mapya  na  mpenzi  mwingine.
Usipende  kusikia  jambo  ila  penda  kuwa  mwonaji  wa  jambo  zaidi  na  kuwa  msikilizaji  wa  jambo  zaidi  kuliko  kusikia  au  kuambiwa  jambo  juu  ya  mpenzi  wako.

MAPENZI  NI  UAMINIFU.

BongoSwaggz.Com

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.