'Shika Adabu Yako' Kutoonyeshwa Kwenye TV Stations Nay Wa Mitego Afunguka. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

'Shika Adabu Yako' Kutoonyeshwa Kwenye TV Stations Nay Wa Mitego Afunguka.

Nay
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amesema video yake mpya ya wimbo ‘Shika Adabu Yako’ kutochezwa kwenye runinga sio tatizo, kwani amedai tayari imeshafika pale alipohitaji ifike.

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Nay alisema video hiyo ambayo audio yake ilifungiwa na Basata kutokana na kukiuka maadili, tayari imevunja rekodi za video za wasanii wa Hip hop zilizoangaliwa zaidi kwa muda mfupi kupitia youtube.

“Kuna baadhi ya TV kama tatu hivi nilisikia zilionyesha. Lakini hii video pia sikuisambaza kwenye TV niliiachia kwenye mitandao na bahati nzuri imeanya poa,” alisema Nay.

Aliongeza, “Unajua huu wimbo tayari Basata walishatoa taarifa kwamba ufungiwe lakini mimi sikupata taarifa rasmi. Kwa hiyo mimi sikutaka kuwadissapoint mashabiki wangu kwenye video, ndio maana video imeanza kuiachia youtube na bado inafanya poa tena huwenda ndio video iliyo ongoza kwa kuangaliwa kwenye youtube kwa wasanii wa Hip Hop. Kwa hiyo mimi naona nimefikia yale matarajio yangu kazi unaenda poa sana kwa sababu audio inafanya poa zaidi,”

-bongo5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.