Ripoti Ya Daktari 'Maini ya Penny Yameharibika' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ripoti Ya Daktari 'Maini ya Penny Yameharibika'

Majibu ya daktari yamemkatisha tamaa Mtangazaji wa Zouk TV, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ baada ya kuambiwa kuwa, kutokana na unywaji wa pombe kali kupitiliza, maini yake yameanza kuharibika na asipochukua hatua za haraka hali itazidi kuwa mbaya zaidi.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Penny, hivi karibuni mrembo huyo aliyewahi kuwa mwandani wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alikuwa hajisikii vizuri na mara nyingi alipokuwa akijaribu kula, alitapika na kuishiwa nguvu hivyo akaamua kwenda kupima kwenye Hospitali ya AAR jijini Dar.
Mpashaji huyo alidai kwamba baada ya Penny kuchukua vipimo vyote, ilibainika kwenye maini yake kuna tatizo na chanzo chake ni unywaji wa pombe kali.“Maskini Penny, sasa hivi hana raha kabisa tangu daktari amwambie ana matatizo kwenye ini, mara nyingi anakuwa mnyonge na mwenye wasiwasi sana,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupokea taarifa hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Penny ambapo alizungumza kwa upole kuwa angeomba vitu vingine asiviweke wazi kwenye vyombo vya habari kwani ni mambo ya kidaktari zaidi.
“Kiukweli sijisikii vizuri na hata kuongea sana naona shida. Unajua vitu vya kidaktari siyo vizuri kuviweka kwenye vyombo vya habari. Kifupi sipo vizuri,” alisema Penny akionekana kutokuwa na furaha.
-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.