Picha: Sugu Aonyesha Maandalizi ya Ujenzi wa Hoteli Yake Huko Mbeya. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Picha: Sugu Aonyesha Maandalizi ya Ujenzi wa Hoteli Yake Huko Mbeya.

Bet Sasa
Msanii mkongwe wa Hip Hop na mbunge wa Mbeya mjini, Mh Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameachia wimbo wake mpya ‘Freedom’ ambapo ndani ya wimbo huo amezungumzia mambo mbalimbali yakiwemo mafanikio yake.
Mkurugenzi wa Hotel Desderia Co Ltd, Mr Joseph Mbilinyi na Eng. Chao Nan wa kampuni ya ukandarasi Home Africa Investment Co Ltd ya China wakisaini mkataba wa ujenzi.

Katika kibao hicho kilichoandaliwa katika studio za MJ Record chini ya producer Marco Chali, Sugu ameelezea jinsi alivyoweza kupambana mpaka kufanikiwa huku alionyesha zaidi kumshukuru mama yake.

Katika ‘Verse’ ya pili ya wimbo huo, Sugu amesema “Mama i made it, mwanao nimefika mbali, maisha yana afadhali nakomaa ili nisifeli, kiukweli hata mwenyewe najikubali najenga mpaka hoteli!,” .

Pia hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa instagram alipost picha ya ujenzi wa hoteli hilo na kuandika: Mkurugenzi wa Hotel Desderia Co Ltd Mr Joseph Mbilinyi na Eng. Chao Nan wa kampuni ya ukandarasi Home Africa Investment Co Ltd ya China wakisaini mkataba wa ujenzi. Kampuni hiyo itajenga hotel ya nyota 3 itakayoitwa Hotel Desderia jijini Mbeya na ujenzi unaanza mara moja kwa mkopo wa bank ya CRDB.
Itakavyokuwa hoteli ya Sugu

Katika post nyingine ya hivi karibuni aliandika: Mkurugenzi wa Hotel Desderia Co. Ltd ya jijini Mbeya Joseph Mbilinyi akiwa kwenye makabidhiano ya site na wakandarasi wa Home Africa Investment Corp Ltd ya China… Mchakato wa ujenzi wa hotel hiyo ya nyota 3 umeanza rasmi leo… Mungu aendelee kubariki. Amen.
Sugu akizungumza na wakandarasi

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.